Wananchi kaunti ya TaitaTaveta sasa wanaweza kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Kampuni ya kusambaza maji Tavevo Water And Sewerage Company Limited kupitia njia ya kidigitali, baada ya Kampuni hiyo kuzindua rasmi huduma hiyo ambapo wananchi wanaweza kupata huduma ,kutoa ripoti ikiwemo wizi wa maji ama uharibifu wa miundomisingi ya maji kupitia,Tavevo Maji App.
Governor Andrew Mwadime – Wakujaa,ambaye ameongoza uzinduzi huo amesema,hatua hiyo inalenga kuimarisha na kurahisisha utoaji wa huduma.
“Njia tuliofuata itarahisisha utoaji huduma na wateja wetu watakua wanatufikia kwa urahisi bila kupoteza mda kuja afisini”amesema Gavana Wakujaa.
Aidha ameongeza kua, kila mteja atakuwa akilipa maji aliyotumia baada ya kufutiliwa ada ya kila mwezi (standing charge) ya shillingi 380.
Waziri wa Maji kwenye kaunti Granton Mwandawiro amesema wizara hiyo inaendelea kuweka mikakati imara ya kuhakikisha wananchi wanapata maji kila siku ikiwemo ujenzi wa tanki za maji , sawa na kuimarisha kuweka mifereji ya kisambaza maji(service lines)
Mkurugenzi wa Tavevo Richard Kibengo kwa upande wake amesema kampuni hiyo inaendelea kuimarisha misingi yake lengo kuu ikiwa kuafikia mahitaji ya wateja wake.
Ili kupata huduma za kampuni ya TAVEVO mteja anahitajika kubonyeza *873*55# kwa simu yake kisha afuate magizo.